
Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids, ameonyesha furaha baada ya timu kufuzu kwa hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku wakibakiwa na mchezo mmoja mkononi. Hata hivyo, Kocha Fadlu alisisitiza kuwa walistahili kupata ushindi mkubwa zaidi katika mechi dhidi ya Bravos Do Marquis.
Fadlu alisema, "Tumepiga mashuti 26 kuelekea lango la Bravos na tumetengeneza nafasi nyingi ambazo zilitakiwa kutupa ushindi mkubwa. Lakini, haikuwa hivyo ingawa tulidhibiti kila kipengele uwanjani."
Pamoja na changamoto za kutokufunga mabao mengi, Fadlu aliwapongeza wachezaji wake kwa kujituma, benchi la ufundi kwa maandalizi bora, na Idara ya Utabibu kwa kuhakikisha kila mchezaji yuko tayari.
"Tuna safari ndefu mbele, lakini mafanikio haya ni hatua muhimu kuelekea malengo yetu ya msimu," aliongeza Fadlu.
Tazama video kamili ya Kocha Fadlu akitoa maoni yake na kuwapongeza mashabiki wa Simba SC kwa sapoti yao kubwa.
Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa habari za hivi punde kuhusu safari ya Simba SC kwenye mashindano ya kimataifa! 🔴⚪
Kocha Fadlu Davids Asema Simba SC Walistahili Ushindi Dhidi ya Bravos

You Might Also Like
06 minute read
Top Story

06 minute read
241 Views



